Tanzania Police Jobs: Jeshi la Polisi Tanzania katika mwaka wa fedha


Jeshi la Polisi Tanzania katika mwaka wa fedha 2013/2014 litaajiri wahitimu wa
vyuo vya Ufundi Stadi nchini na Vyuo vya Mafunzo ya Amali Zanzibar.

Wahitimu wa fani hizo wawasilishe maombi yakiambatanishwa na vivuli vya vyeti
kwa Inspekta Jenerali wa Polisi, Makao Makuu ya Polisi, S. L. P. 9141, Dar es
Salaam kwa kujaza fomu ya maombi iliyowekwa kwenye tovuti ya Jeshi la Polisi www.policeforce.go.tz Fomu
za maombi baada ya kupokelewa, zitachambuliwa wenye sifa wataitwa kwenye usaili
kwa tarehe zitakazotangazwa kwenye vyombo vya habari. Baada ya usaili majina ya
waliofaulu yatatangazwa na watatakiwa kuhudhuria mafunzo ya awali katika Chuo
cha Taaluma ya Polisi Moshi.
Sifa za Mwombaji:-

1. Udereva.

    Awe Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
    Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 25.
     Awe amemaliza kidato cha nne au cha sita na kufaulu.
     Awe amemaliza kidato cha nne na kuendelea katika kipindi
cha mwaka 2010, 2011 au 2012.
     Awe na cheti cha ufundi magari(Automobile engineering au
Transport Management and logistics) yaani NTA level 2 au 3 au 4
     Awe na leseni ya udereva daraja “D”, “E” au “C”.
     Awe na cheti halisi cha kuzaliwa, kuhitimu elimu ya
sekondari, na cheti cha taaluma.
     Awe na tabia njema na asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
     Awe na afya njema itakayothibitishwa na daktari wa
Serikali.
     Awe hajaoa, hajaolewa au kuwa na mtoto.
     Asiwe na alama za kuchora mwilini(Tatuu).
     Awe na urefu usiopungua sentimita 155.
     Awe hajawahi kutumia madawa ya kulevya.
     Awe amefaulu usaili.
     Awe tayari kufanyakazi mahali popote Tanzania.

2. Fundi rangi za magari(Spray and Painting/Panel Beating)
Sifa za Mwombaji:
(i) Awe na cheti cha ufundi rangi za magari yaani NTA level 2 au 3 au 4.
(ii) Sifa zilizotajwa hapo juu isipokuwa sifa ya kuwa na cheti cha ufundi
magari na kuwa na leseni.

3. Fundi wa Matengenezo ya Magari Makubwa(Auto Mechanics– Heavy Duty)
Sifa za Mwombaji:
(i) Sifa zote zilizotajwa kwenye namba moja hapo juu.

4. Fundi wa Matengenezo ya Umeme wa Magari(Auto Electrical)
Sifa za Mwombaji:
(a) Awe na cheti cha ufundi wa matengenezo ya umeme wa magari yaani NTA level 2
au 3 au 4. Au,
(b) Awe na Stashahada ya Ufundi wa Matengenezo ya Umeme wa Magari yaani NTA
level 5 au 6.
(c) Sifa zilizotajwa kwenye namba moja hapo juu isipokuwa sifa ya kuwa na cheti
cha ufundi wa magari na kuwa na leseni.
5. Fundi wa Matengenezo ya Jenereta
Sifa za Mwombaji:
(i) Awe na cheti cha matengenezo ya Jenereta yaani NTA level 2,3au 4. Au,
(ii) Awe na Stashahada ya Matengenezo ya Jenereta yaani NTA level 5 au 6.
(iii) Sifa zilizotajwa kwenye namba moja hapo juu isipokuwa sifa ya kuwa na
cheti cha ufundi wa magari na kuwa na leseni.

6. Fundi Seremala
Sifa za Mwombaji:
(i) Awe na cheti cha Ufundi seremala yaani NTA level 2 au 3 au 4.
(ii) Sifa zilizotajwa kwenye namba moja hapo juu isipokuwa sifa ya kuwa na
cheti cha ufundi wa magari na kuwa na leseni.
7. Fundi Ushonaji
Sifa za Mwombaji:
(i) Awe na cheti cha Ufundi Ushonaji yaani NTA level 2 au 3 au 4.
(ii) Sifa zilizotajwa kwenye namba moja hapo juu isipokuwa sifa ya kuwa na
cheti cha ufundi wa magari na kuwa na leseni.

8. Fundi Matengenezo ya Kompyuta.
Sifa za Mwombaji:
(i) Awe na cheti cha Matengenezo ya kompyuta yaani NTA level 2, 3 au 4.
(ii) Sifa zilizotajwa kwenye namba moja hapo juu isipokuwa sifa ya kuwa na
cheti cha ufundi wa magari na kuwa na leseni.

9. Fundi Matengenezo ya Pikipiki.
Sifa za Mwombaji:
(i) Awe na cheti cha Matengenezo ya Pikipiki yaani NTA level 2, 3 au 4.
(ii) Sifa zilizotajwa kwenye namba moja hapo juu isipokuwa sifa ya kuwa
na cheti cha ufundi wa magari na kuwa na leseni.

Muhimu: Mwisho wa kupokelewa kwa fomu za maombi ni tarehe 15.09.2013.
Hairuhusiwi kuwasilisha fomu ya maombi kwa mkono. Tuma kwa
posta kupitia anuani tajwa.

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x