. Ofisi ya Waziri
Mkuu, Kazi, Aira, na Wenye Ulemavu (OWM-KVAU) inatekeleza program ya kukuza
stadi za kazi nchini ya miaka mitano 2016-2021 amabayo imelenga kuwezesha nguvu
kazi ya Taifa kupata ujuzi na kazi stahiki ili kumudu ushindani katika soko la
ajira. hivyo OWM-KVAU imeingia makubaliano na Taasisi ya Teknolojia Daer es
Salaam ya Mwanza kutoa mafunzo ya stadi za kutengeneza viatu vya ngozi na
bidhaa za ngozi. lengo ni kuhahikisha nchi inakuwa na nguvu kazi ya kutosha
yenye ujuzi unahoitajika katika soko la ajira katika kutengeneza bidhaa za
ngozi nchini
2. Ofisi inapenda
kutangaza nafasi 1000 za mafunzo yatakayoanza ifikapo tarehe 30 February 2017,
katika Taasisi ya Tekinolojia Dar es Salaam kampasi ya Mwanza. vijana
wakitanzania wenye elimu ya msingi na kendelea na umi kati ya miaka 18 hadi 35
wanaopenda kujiunga na mafunso wawasilishe maombi yao kuanzai tarehe 22/012017
hadi 04/02/2017 yakiambatanishwa na nyaraka zifuatazo
i) barua ya maombi yenye anuani kamili ikiwa na namba za simu pamoja na barua
pepe
ii) nakala ya cheti cha elimu uliyohitimu
iii) nakala ya cheti cha kuzaliwa au kadi ya mpiga kura
iv) barua ya utambulisho kutoka serikali za mitaa unayoishi
v) picha 4 za passport
3. maombi
yawasilishwe kwa
MKUU WA KAMPASI,
TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM – KAMPASI YA MWANZA,
S.L .P 2525,
MWANZA
AU KWA BARUA PEPE This email address is being protected from spambots. You need
JavaScript enabled to view it.